Naibu kiongozi wa upinzani bungeni ambaye pia ni waziri kivuli wa Fedha Zitto Kabwe kesho atawasilisha bajeti mbadala ya upinzani bungeni.
Macho na masikio ya watanzania yanatarajiwa kushuhudia kile kilichoandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo kama majibu kwa bajeti ya serikali iliyosomwa na waziri wa fedha William Mgimwa.Bajeti hiyo ya serikali inapingwa kila kona ya nchi kutokana na serikali kujitengea asilimia 70% ya bajeti hiyo kwa matumizi yake huku miradi ya maendeleo ikitengewa tu asilimia 30%
Watu kadhaa waliohojiwa wanasema wanategemea CDM kupeleka bajeti mbadala itakayowakilisha maoni halisi ya wananchi.CDM ambayo kwa sasa inaungwa mkono na idadi kubwa ya watanzania itazidi kujikita mioyoni mwa wananchi kutokana na bajeti mbadala itakayowasilishwa na mbunge wake machachari Zitto Kabwe.
Habari za uhakika kutoka ndani ya CDM zinadai bajeti mbadala imeandaliwa kwa ustadi mkubwa ili kuwaonyesha wananchi CDM itafanya nini itakapoingia madarakani.Tayari kiongozi wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa alishasema chama chake kitatumia kila njia kuipinga bajeti hii kwa manufaa ya watanzania wote.
No comments:
Post a Comment