GERMANY 2-NETHER LAND 1
Ujerumani imedhihirisha ubora wake katika mashindano ya Uero 2012 baada ya kuifunga uholanzi magoli mawili kwa moja.Mshambuliaji Gomez alikuwa mwiba katika ngome ya uholanziIlikuwa dakika ya 24 na 38 Gomez kuwafungia Ujerumani magoli ya kuongoza, kuwapa shangwe mashabiki wa Ujerumani.Dakika ya 73 Van Persie alifunga goli la kufutia machozi kwa upande wa uholanzi. Kutokana na matokeo hayo timu ya Uholanzi inashika mkia katika kundi hilo baada ya kufungwa mechi zote mbili.Mechi ya kwanza walifungwa goli moja na Denmark, hivyo kujiweka katika mazingira mabaya ya kuendelea na mashindano hatua ya robo fainali.
No comments:
Post a Comment