Baada ya Katibu wa baraza la wazee wa klabu ya yangu, mzee Akilimali maarufu kama Abromovich kutoa shutuma nzito kwa mtangazaji wa clouds
fm, Shaffi Dauda Siku ya Jumatatu, tarehe 18, June, 2012, kuwandio kikwazo
cha ujio wa kocha wa kimataifa wa Brazil, Marcio Maximo kuja kuifundisha klabu
ya Yanga.
Sakata limechukua sura mpya baada ya Shaffi Dauda,kutoa tamto kwamba
anampa siku saba (7) Mzee Akilimali kutoa ushahidi au vielelezo vya
shutuma alizomtupia alivyodai anavyo ili kuweza kuthibitisha madai yake dhidi
yake,na kama akishindwa basi itabidi aitishe tena mkutano wa waandishi wa
habari kama alivyofanya wakati akitoa tuhuma zake dhidi yake na akanushe aliyoyasema na kumuomba radhi la sivyo sheria
itachukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment