Search;

Tuesday, June 12, 2012

Mkuu wa Polisi afutwa kazi Afrika Kusini

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amemfuta kazi mkuu wa polisi Generali Bheki Cele, aliyekuwa ametuhumiwa kwa makosa ya rushwa. Bwana Zuma aliambia waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake na pia kuhusu atakayechukua nafasi yake akiwa ni bi Mangwashi Phiyega. Hatua hii inamfanya bi Mangwashi kuwa mkuu wa kwanza wa polisi mwanamke. Generali Cele, ambaye mtangulizi wake alifungwa jela kwa tuhuma za ufisadi, alihukumiwa mwezi Oktoba baada ya taarifa kuhusu kuhusika kwake katika kashfa uuzaji haramu wa nyumba za polisi ingawa alikanusha madai hayo.

No comments:

Post a Comment