Search;

Thursday, June 21, 2012

PINDA AUNDA KAMATI


WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameunda Kamati Maalum ya mawaziri sita kusaidia mchakato wa marekebisho ya Bajeti ya Serikali ambayo mjadala wake utahitimishwa kesho.Kuundwa kwa kamati hiyo kunazifanya kamati zinazoifanyia kazi Bajeti ya 2012/2013 kufikia tatu.

Ijumaa iliyopita wabunge wa CCM waliunda kamati ndogo kwa ajili ya kusaidi pamoja na mambo mengine kuangalia vyanzo vingine vya mapato na kuona iwapo bajeti ya maendeleo inaweza kuongezwa, kukidhi kiu ya wabunge.

Kamati nyingine ni ile ya Fedha na Uchumi ya Bunge ambayo tayari imetoa maoni yake bungeni kuhusu Bajeti, lakini ikabainisha kuwapo kwa kasoro kadhaa ambazo zinapaswa kurekebishwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alikiri kuundwa kwa kamati hiyo, lakini akakataa kutoa taarifa za kina kuhusu suala hilo kwa maelezo kwamba huo ni utendaji wa kawaida wa shughuli za Serikali.

“Sidhani kama hiyo ni habari kubwa ya kwenda kwenye public (kwa umma). Kwanza siyo kamati ya mawaziri, haiwezi kuwa hivyo, na huo ni utendaji wa kawaida wa ndani ya Serikali maana sisi tuna mambo mengi tunafanya,”alisema Lukuvi na kuongeza:

“Kamati za utekelezaji wa shughuli za Serikali ziko nyingi sana na siyo tu za Bajeti. Kwa hiyo ndio maana nakwambia hilo ni jambo dogo sana ambalo mimi sidhani kama linahitaji kutangazwa, kama lingekuwa hivyo mimi ningekuwa wa kwanza kutaka kulizungumzia,” alisema.

Kazi ya Kamati

Habari ambazo Mwananchi limezipata zinasema kwamba kamati ya mawaziri nayo inafanya kazi ya kubuni vyanzo vingine vya mapato ya Serikali, ili kufidia pengo la baadhi ya kodi ambazo zinatarajiwa kufutwa kutokana na shinikizo la wabunge.

Miongoni wa kodi hizo ambazo huenda zikafutwa wakati Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa atakapohitimisha Bajeti yake kesho, ni ile inayopendekezwa kuongezwa kwenye muda wa maongezi ya simu na ile ya inayopendekezwa kutozwa kwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda.

Kadhalika, kamati hiyo ya mawaziri imepewa jukumu la kuona iwapo itaweza kushauri uwezekano wa kuongezwa Bajeti ya sasa ya maendeleo kutoka asilimia 30 inayopendekezwa na Serikali, jambo ambalo pia limekuwa likipigiwa kelele na wabunge wengi.

“Hatuwezi kufumua Bajeti nzima ila kusema kweli ni kwamba lazima kutakuwa na mabadiliko mengi, tatizo kubwa ambalo linatuumiza vichwa, tunajiuliza kama tunaweza kupata hiyo nyongeza ya hizo fedha za maendeleo walau Sh500 bilioni,”alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.

Taarifa zaidi zimewataja wajumbe wanaounda kamati hiyo ambayo ilifanya kikao chake cha kwanza juzi kuwa ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk Mgimwa, Lukuvi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.

Wengine katika kamati hiyo iliyoundwa kwenye kikao cha kazi cha Baraza la Mawaziri, Jumamosi iliyopita chini ya Pinda, ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Naibu Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Adam Malima na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Habari zaidi zilidai kuwa mawaziri hao watafanya kazi hiyo sasa na hata baada ya Bunge la Bajeti ili ushauri wao uweze kuzingatiwa katika maandalizi ya bajeti ijayo ya 2013/2014.

“Tunawatarajia kwamba watatusaidia hata katika bajeti za kisekta zinazokuja,” alisema mjumbe mwingine wa kikao hicho.

Wasiwasi ulikuwa ni iwapo ushauri wa kamati hiyo utaweza kuzingatiwa katika majumuisho ya Waziri wa Fedha na Uchumi wakati atakapohitimisha Bajeti yake, lakini jana Spika wa Bunge, Anne Makinda alifungua milango inayowezesha Serikali kuongeza vyanzo vipya vya mapato hata baada ya Bajeti Kuu kupitishwa.


Wednesday, June 20, 2012

Mzee Akilimali apewa siku saba

Baada ya Katibu  wa baraza la wazee wa klabu ya yangu, mzee Akilimali maarufu kama Abromovich kutoa shutuma nzito kwa mtangazaji wa clouds
fm, Shaffi Dauda Siku ya Jumatatu, tarehe 18, June, 2012, kuwandio kikwazo cha ujio wa kocha wa kimataifa wa Brazil, Marcio Maximo kuja kuifundisha klabu ya Yanga.

Sakata limechukua sura mpya baada ya Shaffi Dauda,kutoa tamto kwamba anampa  siku saba (7) Mzee Akilimali kutoa ushahidi au vielelezo vya shutuma alizomtupia alivyodai anavyo ili kuweza kuthibitisha madai yake dhidi yake,na kama akishindwa basi itabidi aitishe tena mkutano wa waandishi wa habari kama alivyofanya wakati akitoa tuhuma zake dhidi yake na akanushe aliyoyasema na kumuomba radhi la sivyo sheria itachukua mkondo wake.

Monday, June 18, 2012

FARU WALETWA KUTOKA UINGEREZA


Waziri wa Maliasili na Utallii mwenye shuti nyeusi :Balozi Khamis Kagasheki akipeana mkono na Balozi wa Uingereza nchini,Bi Dianne corner baada ya kumkabidhi  faru weusi watatu.Faru hao weusi watatu watapelekwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ikiwa jitahada ya serikali kuongeza idadi ya wanyama hao adimu nchini Tanzania,

Hii si mara ya kwanza kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuleta faru weusi nchini,kwa mara ya kwanza faru walitoka nchini Afrika Kusini lakini baada ya muda mfupi faru hao waliopata umaarufu  waliuawa na majingili.Kwa mantiki hiyo Wizara ya Maliasili na Utalii inabidi iwe macho kwa kuwakea ulinzi   ili wasiuawe na majangili.

Sunday, June 17, 2012

OFFICIAL:ARSENAL KUMUUZA VAN PERSIE

Klabu ya arsenal inayoshiriki ligi kuu ya uingereza imekubali kumuuza mshambuliaji wake van persie kwa paundi millioni 30, hii inakuja siku chache  baada ya kushindwa kufikiana  makubaliano kati ya mchezaji huyo na wamiliki wa klabu hiyo.Klabu inataka kumuuza ili wapate fedha za kuwasajili wachezaji wengine ambao wanahitaji klabuni kwa udi na uvumba.

Klabu za Manchester city na Juventus zote kwa pamoja zikihitaji sahini ya mshambuliaji huyo wa Arsenal na timu ya taifa ya Uholanzi.Klabu ya Manchester city ipo tayari kutoa kiasi cha pesa ili kumsainisha mchezaji huyo aliyemaliza msimu wa 2O11-2012 kinara wa kufumania nyavu katika ligi kuu ya uingereza,ili  kutimiza hiyo klabu hiyo ina mpango wa kuwauza washamulijia wake Tevez na Dzeko.

Zitto kuwasilisha bajeti ya upinzani kesho

Naibu kiongozi wa upinzani bungeni ambaye pia ni waziri kivuli wa Fedha Zitto Kabwe kesho atawasilisha bajeti mbadala ya upinzani bungeni.
Macho na masikio ya watanzania yanatarajiwa kushuhudia kile kilichoandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo kama majibu kwa bajeti ya serikali iliyosomwa na waziri wa fedha William Mgimwa.Bajeti hiyo ya serikali inapingwa kila kona ya nchi kutokana na serikali kujitengea asilimia 70% ya bajeti hiyo kwa matumizi yake huku miradi ya maendeleo ikitengewa tu asilimia 30%
Watu kadhaa waliohojiwa wanasema wanategemea CDM kupeleka bajeti mbadala itakayowakilisha maoni halisi ya wananchi.CDM ambayo kwa sasa inaungwa mkono na idadi kubwa ya watanzania itazidi kujikita mioyoni mwa wananchi kutokana na bajeti mbadala itakayowasilishwa na mbunge wake machachari Zitto Kabwe.
Habari za uhakika kutoka ndani ya CDM zinadai bajeti mbadala imeandaliwa kwa ustadi mkubwa ili kuwaonyesha wananchi CDM itafanya nini itakapoingia madarakani.Tayari kiongozi wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa alishasema chama chake kitatumia kila njia kuipinga bajeti hii kwa manufaa ya watanzania wote.

Saturday, June 16, 2012

NEWS: TWIGA STARS UWANJANI LEO

                                                              Kocha Boniface mkwasa


Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake

Kikosi cha   Twiga Stars kinashuka dimbani leo katika uwanja wa Taifa jijini Dares Salaaam kupambana dhidi ya Ethiopia katika mashindano ya kusaka nafasi ya kushiriki Kombe la Africa kwa wanawake.

Mchezo huo ni marudiano baada wa awali kumalizika kwa Twiga stars kufungwa magoli matatu kwa moja,ili waweze kuendelea inabidi washinde angalau goli moja .

STARS YATUA MSUMBIJI

 Kocha Kim Paulsen akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Shamim Nyanduga mara baada ya timu hiyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo

Kocha Kim Paulsen akiwaongoza wachezaji wake baada ya kushuka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa maputo jana, nchini Msumbiji. Taifa Stars itakipiga na timu ya Msumbiji The Mambas Jumapili, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Afrika Kusini mwaka ujao.


Taifa Stars imewasili Maputo saa 5 asubuhi kwa saa hapa tayari kwa mechi dhidi ya Msumbiji (The Mambas) na kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi Nyandugu.


Stars yenye kikosi cha wachezaji 20 chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen imefikia Hotel 2010 LDA iliyoko karibu na Uwanja wa Taifa Zimpeto ambapo mechi hiyo itachezwa Jumapili kuanzia saa 9 kamili kwa saa za hapa ambapo Tanzania itakuwa saa 10 kamili.


Kwa mujibu wa programu ya Kocha Kim, timu itafanya mazoezi leo na kesho katika muda ule ule wa mechi ya Jumapili ambayo itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar. Mpaka timu inawasili hapa hakuna mchezaji yeyote mwenye matatizo ambayo yanaweza kusababisha asicheze mechi ya Jumapili.



Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Thursday, June 14, 2012

MJENGO WA WEMA UTATA











                                                     Unavyoonekana kwa ndani

Mwigizaji wa filamu Tanzania Wema Sepetu ameanika mjengo wake uliopo kijitonyama ambao umekamilika kila kitu.

DI MATEO KUINGOZA CHELSEA



Kocha Di Mateo amepata mkataba wa miaka miwili ya kuingoza klabu ya chelsea baada ya kuingoza vizuri msimu wa mwaka 2011-2012 na  kupata makombe mawili ya FA na klabu bingwa  Ulaya.Di Mateo amerudi uingereza baada ya kuwa mapumziko ya kumaliza msimu mwenzi May.

Di Mateo alikuwa anashikilia ukocha kwa muda baada ya kufutwa kazi kwa Boas kutokana na mwenendo mbaya wa chelsea katika mashindano mbalimbali.

UJERUMANI YAINGIA ROBO FAINALI

GERMANY 2-NETHER LAND 1
Ujerumani imedhihirisha ubora wake katika mashindano ya Uero 2012 baada ya kuifunga uholanzi magoli mawili kwa moja.Mshambuliaji Gomez alikuwa mwiba katika ngome ya uholanzi

Ilikuwa dakika ya 24 na 38 Gomez kuwafungia Ujerumani magoli ya kuongoza, kuwapa shangwe mashabiki wa Ujerumani.Dakika ya 73 Van Persie alifunga goli la kufutia machozi kwa upande wa uholanzi. Kutokana na matokeo hayo timu ya Uholanzi inashika mkia katika kundi hilo baada ya kufungwa mechi zote mbili.Mechi ya kwanza walifungwa goli moja na Denmark, hivyo kujiweka katika mazingira mabaya ya kuendelea na mashindano hatua ya robo fainali.

Ureno Yaua Uero 2012



                                      DENMARK 2-PORTUGAL 3

Katika mwendelezo wa kombe la ulaya 2012 huko Poland -Ukraine,timu ya ureno chini ya mshambuliaji Ronald wameshinda magoli matatu kwa mawili.Ureno ilipigana kufa na kupona kupata goli la mapema ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kumaliza vinara wa kundi hilo baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Ujerumani.
           Kutokana na michezo ya leo kundi B linasomeka kama ifuatavyo

                            Timu           Point
                           Germany      6
                            Denmark     3
                            Portugal       3
                            Uholanzi      0

Karibu Makumbusho ya Majimaji


                                        Hii ni picha ambayo ipo katika Makumbusho ya Taifa ya                        
                                       Vita vya MajimajiSongea.Hii iliwekwa na kuzinduliwa na
                                       wa kwanza   wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Hayati Baba
                                       Mwalimu Julius K Nyerere.Makumbusho hii ipo Songea
                                      mjini karibu na idara ya maji na Tanesco,njoo ujione babu
                                      zetu walivyopigania uhuru wa Tanzania.Makumbusho zipo kwa
                                       ajili ya watanzania sio kwa wageni

Tuesday, June 12, 2012

Chukua hii


Mkuu wa Polisi afutwa kazi Afrika Kusini

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amemfuta kazi mkuu wa polisi Generali Bheki Cele, aliyekuwa ametuhumiwa kwa makosa ya rushwa. Bwana Zuma aliambia waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake na pia kuhusu atakayechukua nafasi yake akiwa ni bi Mangwashi Phiyega. Hatua hii inamfanya bi Mangwashi kuwa mkuu wa kwanza wa polisi mwanamke. Generali Cele, ambaye mtangulizi wake alifungwa jela kwa tuhuma za ufisadi, alihukumiwa mwezi Oktoba baada ya taarifa kuhusu kuhusika kwake katika kashfa uuzaji haramu wa nyumba za polisi ingawa alikanusha madai hayo.

HAKI ZA WANYAMA

Picha mtu akimkamata mbwa kwa ustarabu:

                                          Shirika la kutetea  haki za wanyama dunian,wametoa
                                          njia mbalimbali za kuwakamata wanyama.Watu wengi
                                          wanapenda kuwanyaynasa  wanyama hii inatokana kutoeleawa
                                             haki za wanyama.

Chadema kuwasha moto


Mbunge Joshua Nassari akisalimia wananchi


Kutokana na mwamko wa wananchi wengi katika masuala ya siasa,chama cha
Demokrasia na Maendeleo (chadema) kinajiandaa kuchukua nchi mwaka 2015.
Hii inatokana na  wananchi kuchoshwa  kusikiliza sera za uongo kutoka CCM